Registration Form for Kirumba Members Only

Kwaya ya kanisa la Waadventista wa Sabato Kirumba (KAC) imekuwa na kawaida ya kuandaa tamasha la uimbaji (hymns festivals) kila mwaka ambapo hadi Desemba 2023 kwaya ilikuwa imefanya matamasha 3 na mwaka huu litafanyika tamasha la 4 ambalo litakuwa la kihistoria la aina yake kwa mtindo tofauti. 

Tamasha la mwaka huu litahusisha waimbaji na washiriki wa zamani kutoka kokote waliko (ndani au nje ya nchi)  waje Kirumba  waungane nasi ambapo kwa pamoja kusanyiko hilo lilete hisia hisia za wimbo mpya wa watakaokombolewa na kurithi makao ya amani mbinguni, kielelezo cha shangwe ya mbinguni tutakapokusanyika  kama familia moja ya Mungu. 

Tamasha hilo litaanza kwa program mbalimbali tangu 23/12/2024 na litafikia kilele chake Sabato ya tarehe 28/12/2024 katika kanisa la Waadventista wa Sabato Kirumba.